January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga hoi kombe la Mapinduzi wavuliwa ubingwa, Azam FC yatinga fainali

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga imevuliwa rasmi ubingwa wa kombe la Mapinduzi mara baada ya kuondolewa na Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali wa michuano hiyo inayofanyika visiwani Zanzibar. Aanaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ulipigwa leo tarehe 1o Januari 2022, majira ya saa 10:15 kwenye dimba la Uwanja wa Aman na kisha kufuatiwa na mchezo kati ya Simba dhidi ya Namungo Fc uliopigwa majira ya saa 2:15.

Yanga imeondoshwa kwenye mchezo huo kwa njia ya mikwaju ya Penati 9-8, kufuatia kumaliza dakika 90 za mchezo bila ya timu hizo kufungana.

Ushindi huo wa Azam Fc umeonekana kama kulipa kisasi kufuatia kuondoshwa katika michuano hiyo kwa njia ya penati kwenye msimu uliopita na klabu ya Yanga na kufanikiwa kutinga fainali na kwenda kutwaa taji hilo.

Katika mapigo hayo ya penati, Yanga ilikosa penati ya nane iliyopigwa na Yassin Mustapha ambayo ilipaa langoni kisha Mudathir Yahaya akamaliza mchezo kwa kuwafungia Azam Fc penati ya tisa na kuiondosha Yanga kwenye michuano hiyo.

Michuano hiyo ya Mapinduzi kwa mwaka huu yalishilikisha timu 10, huku kati ya hizi nne zikitokea Tanzania Bara ambazo ni Azam Fc, Yanga, Namungo FC na Simba.

Timu hizo zote nne zilitoka Tanzania Bara ndio zilizofanikiwa kutika hatua ya nusu fainali kama ilivyo kwa msimu uliopita.

error: Content is protected !!