Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wiki ya nenda kwa Usalama yafutwa
Habari Mchanganyiko

Wiki ya nenda kwa Usalama yafutwa

Spread the love

SERIKALI kupitia Baraza la taifa la usalama barabarani, limetangaza kuifuta sherehe za wiki ya nenda kwa usalama barabarani, iliyokuwa ikifanyika kila mwaka. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Naibu waziri wa mambo ya Ndani, Hamad Yusuf Masauni, amewaambia waandishi wa habari mjini Dodoma, kuwa hatua hiyo ya serikali inatokana na ukweli kuwa sherehe hizo hazijasaidia kuondoa; na au kupunguza tatizo la ajali nchini.

Naibu waziri huyo anasema, “wiki ya usalama barabarani hutumia mabilioni ya shilingi kila mwaka, lakini pamoja na fedha hizo kutumika, bado ajali zimeendelea kuwapo.”

MwanaHALISI Online limeelezwa kuwa tangu Rais John Pombe Magufuli aingie madarakani, Novemba mwaka 2015, amekuwa na utaratibu wa kufuta sherehe kadhaa kwa kisingizio cha kupunguza gharama.

Katika hali ambayo imewaacha wengi mdomo wazi, ni hatua yake ya hivi karibuni ya kufuta sherehe za uhuru wa Tanganyika, zilizokuwa zimepangwa kufanyika tarehe 9 Desemba.

Taarifa iliyotolewa na waziri mkuu wa Jamhuri, Kasim Majaliwa, baada ya Rais John Pombe Magufuli, kuagiza kufutwa kwa sherehe hizo, kiasi cha Sh. 995.1 milioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za uhuru, zielekezwe kwanye hospitali mkoani Dodoma. Sherehe nyingine zilizofutwa, ni sherehe za siku ya Ukimwi duniani.

“Hospitali hiyo itakayojengwa katika eneo la kati ya barabara ya kwenda Hombolo na Chamwino kwenye barabara ya kwenda Dar es Salaam, itakuwa inawahudumia wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wananchi wengine watakaokuwa mkoani humo,”  ameeleza waziri mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!