Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Al-Shabab yaja na idadi waliouwawa Nairobi, Al-Qaeda washangilia
KimataifaTangulizi

Al-Shabab yaja na idadi waliouwawa Nairobi, Al-Qaeda washangilia

Spread the love

KUNDI la kigaidi la Al Shabab linalojinasibisha na Uislam lililofanya mashambulizi jana kwenye moja ya jengo kubwa katika Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi limekuja na idadi yake ya watu waliowauwa. Vinaripoti vyombo vya kimataifa … (endelea).

Kundi hilo limedai kwamba, taarifa ya serikali kuwa, waliofariki kwenye shambulizi hilo lililotokea jana majira ya saa 9 alasiri ni watu sita, si kweli na badala yake waliouwawa ni 47. Mpaka leo tarehe 16 Januari 2019 saa moja asubuhi, milio ya risasi imesikika kwenye jengo hilo.

Baada ya utekelezaji wa shambulio hilo la kinyama, Kundi la Kigaidi wa Al-Qaeda limetoa taarifa ya kufurahia tukio hilo huku likitupa lawama kwa Serikali ya Kenya kwa kupeleka Jeshi lake nchini Somalia kwa madai ya kulinda amani.

Kundi hilo limedai kuwa, Jeshi la Kenya nchini Somalia ni lazima liondoke kwa madai limekuwa likifanya uchafuzi kwa raia wa Somalia. Kenya ilipeleka jeshi lake Somalia mwaka 2011 kukabiliana na Al-Shabab. Jeshi la Kenya limekuwa likishirikiana na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kuisaidia serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa.

Kwenye shambulio hilo lilitokewa katika jengo hilo kubwa lililo na ofisi mbalimbali za kampuni pia hoteli ya kisasasa na ya kifahari ya DusitD2. Taarifa ya idadi ya waliouwawa ya Al-Shabab ilitolewa kwa kupitia mtandao unaounga mkono kundi hilo wa Somali Memo.

Pamoja na mtandao huo kutoa idadi hiyo kubwa ya watu waliouwawa, Serikali ya Kenya haijatoa taarifa yoyote kutokana na madai hayo na badaya yake, wanaendeleza doria kwenye eneo la tukio na vionga vyote vya Nairobi.

Shambulio hilo linakuja ikiwa ni baada ya miaka mitatu la shambulio la aina hiyo lililotokea Garissa na lile lililotokea mwaka 2013 na kusababisha mauaji ya Wakenya 69 kwenye jengo la maduka ya kifahari Westgate Mall.

Fred Matiang’I, Waziri wa Usalama wa Ndani Kenya ameeleza kuwa, majengo yaliyoshambuliwa na kundi hilo la kigaidi yako salama sasana kuwa, wanaelekea kumaliza hatua za mwisho za upekuzi ili kuhakiki kwamba usalama unaimarishwa.

Mashirika na taasisi mbalimbali zimekuwa zikitoa taarifa ya kulaani shambulio hilo ikiwa ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU) ambapo Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo Moussa Faki Mahamat amelaani shambulio hilo.

Robert Godec, Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake Kenya ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.

Kenya imeendelea kuumizwa na kundi hilo hata nje ya mipaka yake. Miaka mitatu iliyopita Kambi ya Jeshi la Kenya nchini Somalia iliyopo el-Adde ilishambuliwa na Al- Shabab na kuua wanajeshi 63 wa Kenya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!