March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dodoma wala Eid leo, wawaonya wafanyabiashara

Spread the love

IMMAMU wa Msikiti wa Alharamain wa Chang´ombe Jijini Dodoma Shaffi Hussein ,amewaasa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei ya vyakula hususan ya mifugo hasa katika sikukuu ya Eid Al haj ili kuwawezesha waumini wengi wa dini ya Kiislam kusherehekea siku hiyo kwa ibada ya kuchinja. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya swala ya Eid Al haj ambayo imerehekewa leo tarehe 21 Agosti, 2018,  Answar Sunn, Immamu wa msikiti huo amesema, kitendo cha kupandisha bei ya mifugo kuelekea siku kuu hiyo kunasababisha waumini wengi wa dini hiyo kushindwa kufanya ibada hiyo ya kuchinja.

“Nawasishi wafanyabiashara wa mifugo wanaotumia sikukuu hii kupandisha bei ya mifugo ,waache tabia hiyo kwa lengo la kuwaweza waislam wengi zaidi kufanya ibada ya kuchinja kama ilivyo maana ya siku yenyewe,” amesema Shaffi.

Aidha amewataka waumini wa dini hiy kusherekea siku kuu hiyo kwa huku wakifuta mafundisho ya Mwenyezi Mungu bila kumkosea.

“Leo ni siku ya furaha,watu wasivuke mipaka katika kusherehekea wakaacha mafundisho ya Mwenyezi Mungu,” amesema.

Awali akitoa mawaidha kwa waumini wa msikiti huo, Ustaadh Muhammad Ramadhani aliwataka waumini hao kusoma na kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu na kuepuka mifarakano katika jamii.

“Siku hizi jamii imekuwa na mifarakano ni kwa sababu watu wameacha kusoma vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu, watu wanavunjiana heshima,” amesema Ustaadh Muhammad.

Baadhi ya waumini wa msikiti huo waliwahimiza waumini wenzao kusherehekea siku hiyo kwa amani, upendo na utulivu miongoni mwa jamii.

Mhasibu wa Msikiti huo, Waziri Abubakari aliwataka waumini hao kuhakikisha kila mtu anakuwa na furaha kama siku yenyewe ilivyo huku wakisaidia yatima na wasiojiweza.

Aidha aliwataka wazazi na walezi kutowapeleka watoto wao katika kumbi ambazo hazina maadili yanayoendana na maadili ya uislam.

Naye Mwalimu, Rajab  Mhina amewataka kushirikiana na kuheshimiana huku wakinywa na kufirahi bila kufanya machukizo mbele za mwenyezi Mungu.

error: Content is protected !!