Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Answar Sunna watoa ujumbe mzito leo
Habari Mchanganyiko

Answar Sunna watoa ujumbe mzito leo

Spread the love

WAISLAM wa Madhuhebu ya Answer Sunna nchi wameungana na Waislamu wengine duniani katika kusherehekea Sikukuu ya Eid Alhaji. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Katiba ibada ya Swala ya Eid iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, mtoa mawaidha baada ya swala hiyo Sheikh Jadu Mcheni amesema, jambo kubwa na ushindi kwa Waislam ni umoja.

Shikh Mcheni amesema kuwa, Waislam watakapokuwa na umoja, hakuna jambo linaloweza kuwayumbisha kutokana na msikamano ulio imara.

Pia ametoa ujumbe wa kushikamana na ibada ya sadaka ambapo ni miongoni mwa mambo muhimu yanayotakatisha vitendo vya muumini mbele ya Mola wake.

“Tunapaswa kukumbuka kutoa sadaka endelezu, huku ndio kupona kwetu mbele ya Allah. Miongoni mwa sadaka tunazotakiwa kuzikimbilia ni kama ujenzi wa nyuma za ibada ama kutoa Waqf,” amesema.

Sheikh Mcheni ameuelezea umma uliofurika kwenye swala hiyo kuwa, pamaoja na mapito ya sasa Waislam wanapaswa kusaidiana.

Ibada ya swala ya Eid leo tarehe 21 Agosti 2018 imeyofanyika baada ya Waislam waliokwenda Hijja, Makka kusimama kisimamo cha Arafa jana Jumatatu na kutekeleza Ibada ya Kuchinja leo Jumanne.

Miongozi mwa nchi za Afrika zilizoswali Swala ya Eid kitaifa ni pamoja na Kenya, Uganda, Burundi, Jamhuri ya Kidemoksia ya Kongo (DRC) na Zambia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Ditopile aungana na Wana-Kongwa kwa Iftar, wamuombea dua Rais Samia

Spread the loveKATIKA muendelezo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mbunge wa Viti...

Habari Mchanganyiko

PSSSF yawekeza kwenye viwanda 4, kuzalisha ajira 3,000

Spread the loveKATIKA kuisaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa ajira nchini,...

Habari Mchanganyiko

Luhemeja ahimiza utunzaji rasilimali maji kwa faida ya vizazi vijavyo

Spread the love  NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja...

Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the loveMFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito...

error: Content is protected !!