Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wadau waitwa kutoa maoni miswada ya sheria
Habari za Siasa

Wadau waitwa kutoa maoni miswada ya sheria

Stephen Kagaigai, Katibu wa Bunge
Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaalika wadau kutoa maoni yao yatakayotumika katika mchakato wa uchambuzi wa miswada ya sheria kwenye ngazi ya Kamati za Bunge. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 21 Agosti, 2018 na Stephen Kagaigai, Katibu wa Bunge kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano Ofisi ya Bunge.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wadau mbalimbali wanakaribishwa kwa ajili ya kutoa maoni yao kwenye Kumbi zilizopo Jengo la Msekwa na Jengo la Utawala katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kuanzia saa 3 asubuhi.

“Katika kutekeleza Masharti ya Kanuni ya 84 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 kuhusiana na umuhimu wa maoni ya Wadau katika mchakato wa uchambuzi wa Miswada ya Sheria katika ngazi ya Kamati za Bunge, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Stephen Kagaigai anautangazia Umma kwamba, Kamati za Bunge zitafanya zoezi la kukusanya maoni ya Wadau mbalimbali kuhusiana na Miswada ifuatayo ya Sheria,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Miswada inayotarajiwa kutolewa maoni ni pamoja na Muswada wa Bodi ya Kitaalam ya Walimu ambapo maoni yake yatapokelewa Alhamisi tarehe 23 Agosti, 2018 na Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Muswada mwingine utakaotolewa maoni ni wa Sheria ya Tamko la Kutangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa MWAKA 2018. Kamati ya Bunge ya Utawa na Serikali za Mitaa itapokea maoni kuhusu mswada huo.

Vile vile, Kamati ya Bunge ya Bajeti itapokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2018 siku ya Jumatatu tarehe 27 na siku ya Jumanne tarehe 28, Agosti, 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

error: Content is protected !!