September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

11 wajitosa Urais Chadema

Spread the love

WANACHAMA 11 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamejitokeza kutia nia ya kugombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Muda wa utiaji nia ulikuwa kuanzia tarehe 3 hadi 15 Juni, 2020 kwa mwanachama yeyote aliyekuwa na nia ya kutia nia, kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema.

Leo Jumatano tarehe 17 Juni 2020, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema, wanachama 11 pekee ndio waliokidhi vigezo vya awali vya utiaji nia .

Amewataja wanachama hao ni; aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Makamu Mwenyekiti wa Chadema- Bara, Tundu Lissu, Dk Mayrose Majinge na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Wengine ni Peter Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Mchungaji Leonard Manyama, Wakili Gasper Mwanalyela, Nalo Opiyo, Wakili Simba Neo na Msafiri Shabani.

Makene amesema, kwa bahati mbaya mwanachama mmoja ameshindwa kukidhi vigezo vya kanuni za uchaguzi za chama hicho na kwamba ameshindwa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Amesema, baada ya kufungwa kwa pazia la utoaji nia, chama hicho kitaendelea na mchakato mwengine ambao utatangazwa.

error: Content is protected !!