October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Hussein Mwinyi ajitosa Urais Zanzibar

Spread the love

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi amejitosa katika kinyang’anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea)

Dk. Mwinyi amechukua fomu ya Urais leo Jumatano tarehe 17 Juni 2020 katika Ofisi za CCM zilizipo Ugunja Zanzibar.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu, alikwenda eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Dk. Mwinyi ambaye ni Mbunge wa Kwahani visiwani Zanzibar amesema, “leo sikuja kuzungumza na waandishi wa habari, nimekuja kuchukua fomu tu na wala sina la kuzungumza.”

Amesema, hajajua kilichomo kwenye hizo fomu, hivyo akaomba aende akazisome kwanza ajue kilichomo.

Dk. Mwinyi amekuwa mgombea wa tano kuchukua fomu akitanguliwa na; Mbwana Bakari Juma, Mbwana Yahya Mwinyi, Omar Sheha Mussa na Balozi Ali Karume ambaye ni Mtoto wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Aman Abeid Karume

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

error: Content is protected !!