Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri wa Fedha atia nchi hasara Mil 80 kila siku
Habari za SiasaTangulizi

Waziri wa Fedha atia nchi hasara Mil 80 kila siku

Dk. Philip Mpango, wakati akiwa Waziri wa Fedha na Mipango 2015-19
Spread the love

KILA siku taifa linateketeza Sh. 80 milioni kulipa wakandarasi kutokana na Philip Mpango, Waziri wa Fedha kushindwa kuruhusu Shirika la Nyumba (NHC), kumalizia miradi yake ya ujenzi wa nyumba. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Miradi hiyo minne ukiwemo ule ya Morocco na Kawe, jijini Dar es Salaam imekwama kwa maelezo kwamba, Waziri Mpango amekataa kutoa kibali cha kupata fedha ili kumalizia miradi hiyo kwa madai, serikali imehamia Dodoma.

Kutokana na hali hiyo, serikali imelazimika kuwalipa wakandarasi wanne kila mmoja Sh. 20 kwa siku, wakisubiri uamuzi wa Waziri Mpango kumalizia ujenzi huo ili watu waanze kupanga ama kununua ili kuanza kurejesha fedha hizo.

Maelezo hayo yametolewa na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema), tarehe 30 Januari 202 huku akimtuhumu Waziri Mpango kusababisha hasara hiyo  kwa taifa.

Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA), ametoa kauli hiyo bungeni alipokuwa akichangia katika taarifa iliyowasilishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Amenyooshea kidole Mpango kwa madai ya kushindwa kuwapa kibali NHC cha kukopa, ili kuweza kuendeleza ujenzi wa miradi ambayo ilitakiwa kujengwa kawe kwa madai serikali imehamia Dodoma.

“Ukiangalia taarifa ya PAC, inaonesha Shirika la Nyumba la Taifa kwa mwaka 2016/17 mapato yalikuwa bilioni 154, na matumizi billion 122 na mwaka 2017/18 mapato yalikuwa bilioni 116 na matumizi bilioni 83.2,” amesema.

Na kwamba, taarifa ya kamati inaonesha dhamira ya kulilaumu shirika zaidi pasipo kuangalia shirika limefikaje hapo.

Amesema, ujenzi wa Nyumba Moroco, jijini Dar es Salaam, ujenzi wa nyumba 711 Kawe umekwama kwa sababu ya Waziri Mpango kugoma kutoa kibali kwa shirika hilo kukopa.

Kutokana na hali hiyo, miradi hiyo imekwama na kusababisha kuwepo kwa hasara ambayo ingeweza kuepukika.

“Mwenyekiti wa PAC alipokuwa anazungumza na Bunge alisema, kutokana na kukwama kwa miradi yote mwaka 2017, serikali inalazimika kumlipa mkandarasi Sh. milioni 20 kila siku na kutokana na hali hiyo, miradi ipo 4 hivyo kila mkandarasi anatakiwa kulipwa Sh. milioni 20 kila siku,” amesema Mdee.

Mdee alisema kutokana na Maelezo hayo kwa miaka mitatu 2017/20 serikali inatakiwa kulipa bilioni 21.6, wakati hakuna kazi yoyote inayoendelea kwa sababu ya Waziri wa Fedha kushindwa kutoa kibali kwa NHC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!