Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkopo WB: Bunge lamuwinda Zitto
Habari za Siasa

Mkopo WB: Bunge lamuwinda Zitto

Spread the love

ZITTO Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), anasubiriwa kwa hamu na Bunge la Jamhuri, kutokana na uamuzi wa kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB), kutaka isitishe mkopo wa elimu kwa Tanzania. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kwa mujibu wa Job Ndugai, Spika wa Bunge leo tarehe 31 Januari 2020, wanamsubiri Zitto ‘atoke huko alipo’ na atakapofika bungeni, atatakiwa kutoa maelezo ya msukumo wake wa kuiandikia barua WB kuzuia mkopo wa Dola za Marekani Mil 500.

“…wakati mwingine mwenendo wetu unakuwa haueleweki, kwa mfano mbunge mwenzetu atakaporudi, anaweza kutufafanulia wenzake, mheshimiwa Zitto Kabwe kuandika barua World Bank kwamba nchi yetu ikose fursa ya mkopo, ambao lengo lake ni elimu kwa sababu ya tofauti za sera ambalo ni jambo la kawaida.

“Mtu unaweza kuwa na utofauti wa sera au mtazamo, kati ya wewe mbunge au upande wa serikali na kadhalika, yani kufikia mahali pa kublock (kuzuia) Tanzania isipate fursa fulani, nadhani nadhani ni kwenda mbali mno,” amesema Spika Ndugai.

Amewaeleza wabunge kuwa, watoto watakaokosa elimu kutokana na mkopo huo ni wa Tanzania, na miundombinu ni ya Tanzania na kwamba, hajui mbunge katika hilo anafaidika nini?

“…na sijui katika hilo kama mbunge anafaidika nini?” amehoji na kuongeza “kwa sababu kama ni tofauti za kisera, haya ni mambo ya kujadili tu, na ndio maana sisi ni wabunge hapa.”

“Kwa kweli limetugusa na kutukera wengi ambao bado hatujaelewa vizuri hili jambo…, wakati baadhi yetu hapa watoto wetu wako Feza Boys, wako Marian Girls halafu unablock (kuzuia) msaada kwa watoto walio wengi, wa wapiga kura wetu,” amesema Spika Ndugai.

Taarifa zilizopatikana leo, zinaeleza kuwa WB, imegoma kutoa mkopo huo, kwa maelezo kwamba lazima Tanzania iruhusu wanafunzi wanaopewa ujauzito, kurudi shuleni baada ya kujifungua.

“Benki ya Dunia itatoa mkopo pale tu katazo la wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni liaondolewa,” imeeleza WB na kuongeza “hakuna mkopo mpya mpaka wanafunzi wa kike wote wataporuhusiwa kuendelea na masomo yao.”

Taarifa hiyo inatokana na kikao kilichofanyika jana tarehe 30 Januari 2020, kilichojadili hatma ya mkopo huo baada ya Zitto na wanaharakati wengine kuitaka WB kusitisha mkopo huo kwa madai ya ubaguzi wa watoto wake kike katika kupata elimu unaofanywa na Serikali ya Tanzania.

Mpaka sasa, serikali haijaeleza chochote kuhusu uamuzi wa WB unaole;ezwa kufikiwa jana baada ya kikao cha mjadala kuhusu mkopo huo kufanyika.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!