WAKILI wa kujitegemea Mchungaji Kuwayawaya Stephen, amesema kuwa viongozi waliopo madarakani katika serikali ya awamu ya tano wengi wao bado hawajaonyesha uwezo wao wa kiutendaji na badala yake wamekuwa wakijificha katika kivuli cha matamko mbalimbali yanayotolewa na Rais John Magufuli, anaandika Mwandishi Wetu.
Kuwayawaya aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya kusimikwa kwake kuwa Askofu kuongoza huduma inayoitwa Grobal Revival Network.
Amesema kuwa viongozi wengi wa serikali katika awamu ya hii ya tano bado hawajafanya kazi kwa uwezo katika nafasi mbalimbali walizopangiwa na badala yake wengi wao wamekuwa wakifanya kazi kupitia kauli mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Rais.
Aidha, alisema kuwa viongozi wengi ambao wameteuliwa katika nafasi zao wameshindwa kufanya kazi kwa kujiamini na hivyo kushindwa kuonyesha uwezo wao.
“Kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera za eneo lake kwani kila wizara ina sera zake na miongozo yake aliyopewa badala ya kusubiri Ra atoe tamko fulani ndipo wanainukia.
Amesisitiza kwamba changamoto nyingine ambayo anaiona katika utawala wa awamu ya tano ni vitendo vya viongozi kuvujisha siri za serikali hali ambayo haitakiwi kuendelea kufumbiwa macho.
Leave a comment