August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UVCCM wang’ata na kupuliza Mwanza

Shaka Hamidu Shaka, Kaimu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)

Spread the love

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umewataka viongozi wa wilaya kuwachukulia hatua watendaji wao wa chini wanaotoa mikpo kwa vikundi hewa, anaadika Mwandishi Wetu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka.

Shaka amewataka Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wao kuwachukulia hatua kali watendaji walio chini yao kwa kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma maendeleo.

Akizungumza katika ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza ambayo imeanzia wilaya za Magu na Ukerewe, Shaka amesema vijana wengi wanashindwa kupata mikopo.

Amesema watendaji wa umma wamekuwa ni tatizo katika kutoa mikopo ya asilimia tano ambayo serikali imekuwa ikitenda kwa vijana na wanawake.

Amesema bado kuna urasimu mkubwa kwa maofisa wanaohusika kutoa mikopo, wanatakiwa kufanya kazi kwa vitendo ili kumuunga mkono rais Magufuli.

Sakata la Makinikia kupunguza kiwango cha Ushuru wa huduma mara mbili kuliko kilichokuwa kinatoa awali.

error: Content is protected !!