Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wagonjwa wa Fistula wasibaki nyumbani
Afya

Wagonjwa wa Fistula wasibaki nyumbani

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI,
Spread the love

WAZIRI wa Afya Tanzania, Ummy Mwalimu amesema Wanawake wenye matatizo ya Fistula wanatakiwa kuacha tabia ya kujifungia ndani na badala yake waende kupata matibabu katika Hospitali zilizoainishwa na Serikali bila gharama yeyote. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na Waandishi wa Habari katika kuadhimisha siku ya Fistula duniani inayoadhimishwa tarehe 23 Mwezi Mei kila Mwaka, yenye kauli mbiu mwaka huu inayosema “Tokomeza unyanyasaji wa kijinsia: Tokomeza huduma ya afya isiyo na usawa; Tokomeza Fistula sasa!” 

Waziri Ummy amesema takwimu za Shirka la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa kuna wanawake takribani 2,000,000 wanaoishi na Fistula Duniani kote. Inakadiriwa kuwa wagonjwa wapya kati ya 50,000 na 100,000 hupatikana kila mwaka, juhudi za kutibu Fistula huishia kutibu wagonjwa 20,000 tu.

Kwa upande wa Tanzania, Waziri wa Afya Ummy amesema inakadiriwa kuwa na wanawake takribani 2500 ambao wanapata fistula kila mwaka, huku idadi ya wanaopatiwa matibabu ikiwa ni takribani wanawake 1,000 na kuongeza kuwa Tanzania imepiga hatua katika matibabu haya.

“Katika kipindi cha miaka Mitano kuanzia 2015 hadi Disemba, 2019 wanawake zaidi ya 5,500 wametibiwa Fistula. Mafanikio haya yanatokana na kampeni iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya Serikali na Wadau ambayo imeweka Mabalozi wa Fistula zaidi ya 3,000 nchi nzima,” amesema.

Waziri Ummy ametaja takwimu zinazoonyesha kuwa idadi ya Wanawake wanaojitokeza kutibiwa Fistula kwenye Hospitaii za CCBRT, Bugando,Nkinga na Kuvulini Maternity Center imepungua kwa zaidi ya 30% kuanzia mwaka 2015 mpaka 2019 Mwaka 2015, wanawake 1337 walipatiwa matibabu ya Fistula.

Mwaka 2016 walikuwa 1356, mwaka 2017 idadi hiyo ikashuka na kufikia 1060, mwaka 2018 ikashuka tena na kufikia idadi ya wanawake 900, na mwaka 2019 ikashuka zaidi na kufikia wanawake 852. Hii imetokana na kuimarika kwa huduma za Afya ya mama wajawazito chini ya awamu ya Tano.

“Mama mjamzito endapo atawahi kliniki mapema kwa ajili ya uchunguzi wa maendeleo ya afya yake na mtoto na kuhakikisha anajifungulia katika kituo cha kutolea huduma za afya atapunguza uwezekano wa kupata tatizo la Fistula,” amesema na kuongeza.

“Nitumie fursa hii kuendelea kuhimiza akina mama wajawazito kuwahi kliniki mapema, kukamilisha mahudhurio yote manne na kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya”.

Huduma za Fistula nchini zinapatikana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, CCBRT, Bugando, Hospitali ya Kanda ya Rufaa-Mbeya, Hospitali ya Nkinga Tabora, KCMC na Kivulini Maternity Center iliyoko Arusha. Tuna wataalamu waliobobea kwenye tiba ya Fistula kwenye Hospitali hizi.

Waziri Ummy amesema ili kutokomeza Fistula nchini kunahitajika juhudi za pamoja za wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa Afya kwenye ngazi zote, Wizara mbalimbali,wadau wa Maendeleo,Wanahabari na Mashirika ambayo yamekuwa yakijihusisha na uhamasishaji wa matibabu ya Fistula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!