Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara Ubungo wacharuka
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara Ubungo wacharuka

Wafanyabiashara wa Kituo cha Mabasi cha Ubungo wakisubiri mkutano na Kamati ya Fedha ya Jiji la Dar es Salaam
Spread the love

MFANYABIASHARA ambaye pia ni Naibu katibu wa Wafanyabiashara kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es salaam, John Shayo ametangaza kuuburuza mahakamani uongozi wa kituo hicho kwa madi kuwa umetafuna fedha za wanazolipa kodi, anaandika, Irene Emmanuel.

Amesema anashangaa kuona anadaiwa deni kubwa la Sh. 800,000 wakati amelipa kodi zote.

“Haki yoyote inapatikana mahakamani, na mimi ninaweza kuwaambia hivi, huyu mtawala wa kituo ambaye ni meneja, mimi ndo nitakaye ‘mface’ zaidi kwa maana ameidanganya halmashauri, nitamfungulia mashtaka mahakamani,” amesema Shayo.

Akiongea na MwanaHALISI Online leo katika ziara ya kamati ya uongozi na fedha ya halmashauri ikiongozwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amesema kuwa mstahiki meya amedanganywa juu ya mikataba ya wapanganaji.

“Mstahiki Meya amedanganywa, nianze kuelezea hilo la mkataba, ule siyo mkataba, ni masharti magumu mno ambayo hawa wenzangu niliowabeba kama kiongozi wao hawawezi kuyatimiza” Shayo alieleza.

Aidha, Mstahiki Meya baada ya ziara hiyo, amewataka wafanyabiashara wote kituoni hapo kulipao madeni yao ya halmashauri hadi kufikia mwezi ujao na wasipotimiza hilo wataondolewa kwa nguvu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!