Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Magari mapya yaja Zimamoto
Habari Mchanganyiko

Magari mapya yaja Zimamoto

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani).
Spread the love

JESHI la Zimamoto na Uokoaji nchini limetengewa Sh. 3 bilioni kwa ajili ya kununulia vitendeakazi zikiwemo gari za kuzima moto na madawa ya kuzima moto. Sehemu ya bajeti ya mwaka mpya wa fedha wa 2017/18, zitatumika kununulia sare za askari wa jeshi hilo, anaandika Mwandishi Wetu.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye amesema bajeti hiyo katika mwaka mpya wa fedha wa 2017/18 ulioanza Julai mwaka huu, ni ongezeko la fedha zilizotolewa katika mwaka wa fedha wa 2016/17 ambazo ni Sh. 1.5 bilioni.

Kamishna Jenerali Andengenye amesema katika taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Ndani, Christina Mwangosi, kuwa bajeti hiyo ni hatua ya utekelezaji wa azma ya serikali kuimarisha huduma za zimamoto na uokoaji nchini.

Huduma hizo zimekuwa zisizotosheleza kiwango, udhaifu ambao miongoni mwa sababu zake ni uhaba wa fedha za bajeti.

Katika kipindi cha bajeti iliyopita, serikali ililipatia kikosi cha zimamoto na uokoaji Sh. 1.5 bilioni ambazo zilinunuliwa magari ya kuzima moto. Lakini kwa mwaka mpya wa fedha serikali imeazimia kutumia Sh. 500 milioni kwa ajili ya ununuzi wa madawa ya kuzima moto.

Kadhalika, Kamishna Jenerali Andengenye amesema kumetengwa Sh. 100 milioni zitakazotumika kununulia sare za askari wa jeshi hilo, hivyo kuondoa tatizo la muda mrefu la upungufu wa sare za kazi kwa askari wa Zimamoto na Uokoaji.

“Jitihada zinazooneshwa na serikali katika kuliimarisha jeshi letu zitaongeza morali kwa viongozi na askari hivyo kuchangia kuliwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi kama yalivyo matarajio ya Watanzania,” amesema Andengenye.

Katika hatua nyingine, Kamishna Andengenye amesema uongozi wa jeshi hilo umejipanga kuongeza kasi ya kushirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali kwa lengo la kujenga mshikamano unaokusudiwa kusaidia kukabiliana na majanga ya moto na ajali nyinginezo nchini.

Amesema hHuduma zinazotolewa na jeshi hilo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu njia za kuzuia majanga ya kibinadamu na kuchukua hatua za kupunguza madhara yanayosababishwa na mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!