Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ukipanda chuki, utavuna chuki – Zitto
Habari za Siasa

Ukipanda chuki, utavuna chuki – Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amesema nchi imevimba usaa wa chuki. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto ametoa kauli hiyo tarehe 22 Oktoba 2019, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Ukijenga matumaini kwa nchi, unavuna vitu vingi, lakini ukipanda chuki, utavuna chuki. Viongozi wajue nchi imevimba usaa wa chuki, wanawajibu wa kutumbua usaha wa chuki uliotunga kwenye nchi yetu,” amesema Zitto. 

Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema, nchi inapitia katika kipindi kigumu, ambacho baadhi ya watu wamefikia hatua ya kufurahia matatizo yanayowapata wenzao wenzao.

Amewataka viongozi kuiondoa hiyo chuki ili Taifa lirudi katika umoja na mshikamano.

“Tuwe na amani, tujibizane, tuwe wamoja tuendeelee kuwa kama watanzania. Ni wajibu wa viongozi kuondoa hiyo chuki ili tuwe wamoja. Mbele ya Mungu hakuna mtu aliyechuma wote ni udongo na tutarudi kwa udongo,” ameeleza Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!