April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ukipanda chuki, utavuna chuki – Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amesema nchi imevimba usaa wa chuki. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Zitto ametoa kauli hiyo tarehe 22 Oktoba 2019, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Ukijenga matumaini kwa nchi, unavuna vitu vingi, lakini ukipanda chuki, utavuna chuki. Viongozi wajue nchi imevimba usaa wa chuki, wanawajibu wa kutumbua usaha wa chuki uliotunga kwenye nchi yetu,” amesema Zitto.¬†

Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema, nchi inapitia katika kipindi kigumu, ambacho baadhi ya watu wamefikia hatua ya kufurahia matatizo yanayowapata wenzao wenzao.

Amewataka viongozi kuiondoa hiyo chuki ili Taifa lirudi katika umoja na mshikamano.

“Tuwe na amani, tujibizane, tuwe wamoja tuendeelee kuwa kama watanzania. Ni wajibu wa viongozi kuondoa hiyo chuki ili tuwe wamoja. Mbele ya Mungu hakuna mtu aliyechuma wote ni udongo na tutarudi kwa udongo,” ameeleza Zitto.

error: Content is protected !!