Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Takukuru nusura wamdake ‘mgombea’ ubunge CCM Ubungo, wanne mbaroni
Habari za SiasaTangulizi

Takukuru nusura wamdake ‘mgombea’ ubunge CCM Ubungo, wanne mbaroni

Spread the love

MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anayejipanga kugombea ubunge katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam (jina tunalo), amewatoroka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika tukio hilo lililotokea jana jioni tarehe 31 Mei 2020, viongozi wanne wa chama hicho katika jimbo hilo, wanashikiliwa na Takukuru wilaya ya Ubungo.

Taarifa ambazo MwanaHALISI Online ilizopata leo Jumatatu tarehe 1 Juni, 2020 zinaeleza, viongozi hao wanatuhumiwa; kutoa rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu Oktoba 2020 kabla ya wakati.

Msiri wa mtandao huu ameeleza, wakati wa mtego huo, mmoja kati yao alikurupuka na kukimbia na kutelekeza gari, kwenye tukio hilo viongozi wanne wamekamatwa.

“Walikuwa na mtu mmoja mmama anayetaka kugombea ubunge Ubungo, lakini yeye alikimbia ila akaacha gari na wenzake wanne ambao ni viongozi mbalimbali jimboni humo wakakamatwa na Takukuru wa Ubungo,” ameeleza.

MwanaHALISI Online limemtafuta Emmanuel Tarmo Boay, Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Ubungo ili kupata ufafanuzi wake, amesema “suala hilo siwezi kulizungumzia mimi, atafutwe Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni ambaye ndiye mzungumzaje wa mkoa.”

Pili Mwakasege, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni alipotafutwa, amesema suala hilo atalitolea ufafanuzi, “tutatoa taarifa rasmi. Tuko kazini.”

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONELINE kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!