November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ratiba Ligi Kuu Bara hadharani

Almas Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB)

Spread the love

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo leo ametangaza ratiba ya michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi daraja la kwanza ambayo intarajia kuanza kupigwa terehe 13 Juni, mwaka huu, kwa michezo miwili kupigwa siku hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Michezo hiyo ambayo imerejea baada ya kauli ya Rais John Magufuli au kuruhusu matukio ya michezo kurejea kutokana na kuwepo kwa mwenendo mzuri wa ugonjwa wa Covid-19 nchini alipokuwa akiwaapisha mabalozi na Naibu Waziri wa Afya Dodoma, Mei 21, 2020.

Ligi hiyo ambayo itachezwa katika mfumo wa nyumbani na ugenini kama ilivyokuwa hapo awali, klabu ya Mwadui wataikaribisha Yanga kwenye uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga, huku Coastal Union wataikabili Namungo, CCM Mkwakwani.

Michezo mingine itakayopigwa tarehe 14 Juni, 2020, klabu ya Simba itavaana na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Azam itamenyana na Mbao FC kutoka Mwanza.

Mpaka sasa klabu ya Simba ndiyo ipo kileleni kwenye msimamo wa Ligi baada ya kujikusanyia pointi 72 na kujiweka mbioni kuchukua taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

error: Content is protected !!