Spika Ndugai amtupia zigo la CUF Msajili wa Vyama – MwanaHALISI Online
Kulia Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Kulia Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Spika Ndugai amtupia zigo la CUF Msajili wa Vyama

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, amesema kuwa mgogoro wa Chama cha Wananchi (CUF) wa sakata la wabunge nane ni utaratibu ulianza kwa Msajili wa Vyama vya siasa nchini na siyo bungeni, anaandika Faki Sosi.

Ndugai leo amewaambia waandishi kuwa bunge haliwezi kutiwa hatiani katika sakata hilo kwani wenye dhamana ya wanachama kutka katika vyama vya siasa ni Msajili wa Vyama vya Siasa.

Ndugai ameeleza endapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haimtambui mwanachama au kiongozi wa chama husika cha siasa naye hatamtambua kiongozi huyo.

“Mwenye kumbukumbu, Katiba na Viongozi halali wa vyombo vya siasa ni Msajili wa Vyama vya Siasa sio mtu mwengine.

“Linapotokea jambo lenye mvutano kazi yangu ni kuumuliza Msajili wa Vyama vya Siasa akisema hamfahamu basi na mimi sitamfahamu,” amesema Ndugai.

Ndugai amesema kuwa amepata barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa Mwezi, mwezi Machi mwaka huu, kwamba Maalimu Seif Sharrif Hamad hayupo Ofisi ndiyo sababu ya kutojibu barua ya katibu huyo.

Hata hivyo Ndugai amesema kuwa kwa wabunge waliopewa adhabu wasijirekebisha adhabu zitaongezeka zaidi kutokana na kuchukua na tabia za wabunge hao.

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, amesema kuwa mgogoro wa Chama cha Wananchi (CUF) wa sakata la wabunge nane ni utaratibu ulianza kwa Msajili wa Vyama vya siasa nchini na siyo bungeni, anaandika Faki Sosi. Ndugai leo amewaambia waandishi kuwa bunge haliwezi kutiwa hatiani katika sakata hilo kwani wenye dhamana ya wanachama kutka katika vyama vya siasa ni Msajili wa Vyama vya Siasa. Ndugai ameeleza endapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haimtambui mwanachama au kiongozi wa chama husika cha siasa naye hatamtambua kiongozi huyo. "Mwenye kumbukumbu, Katiba na Viongozi halali wa vyombo vya siasa ni Msajili wa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Faki Sosi

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube