Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu aachiwa huru kwa dhamana
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu aachiwa huru kwa dhamana

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema akitoka polisi baada ya kuachiwa kwa dhamana
Spread the love

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, ameachiwa kwa dhamana ya Polisi kwa masharti ya kurudi tena polisi Jumatatu ya Agosti 28, mwaka huu, anaandika Hamisi Mguta.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoka kituo cha Polisi Kanda ya Dar es Salaam, wakili wa Lissu, Peter Kibatala amesema tuhuma alizotakiwa kuziandikia maelezo ni za uchochezi na kutoa maneno ya kashfa.

“Kwa kuwa hatujakwenda mahakamani tutajua mbele ya safari lakini masharti ya dhamana anatakiwa kurudi tena tarehe 28,” amesema Kibatala.

Vionjo kuhusu Tundu 

Tarehe 18 Agosti alikutana na waandishi wa habari Hoteli ya Protea Courtyard, Upanga.

Tarehe 19 Agosti Serikali ikajibu kupitia Kaimu Msemaji wake, Zamaradi Kawawa.

Tarehe 22 Agosti alikamatwa akiwa anatoka Mahakama ya Kisutu.

Anapelekwa Central Polise Station. Baada ya maelezo huku Lissu akikataa kuandika maelezo, alilala huko.

Tarehe 23 Agosti anapelekwa nyumbani kwake kusachiwa.

Tarehe 24 Agosti anapelekwa kuandika dhamana ya maandishi ya Polisi.

Lissu ambaye wamili wake Peter Kibatala anasema anadaiwa kuwa amemkashifu rais kwa kuyasema makosa yake hadharani na amefana uchochezi kuhusu taarifa ya Bombadier kushikiliwa nchini Canada kwa deni, hajapelekwa mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!