March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hatma ya wabunge nane wa CUF kula kiapo kutolewa leo

Wabunge wa CUF wakizungumza na Wakili wao Peter Kibatala walipokuwa katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam

Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajiwa kutoa uamuzi wa kuapishwa wabunge wanane walioteuliwa na Profesa Ibrahim Lipumba au wasiapishwe, anaandika Faki Sosi.

Kwa mujibu wa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Septemba 5, mwaka huu wabunge wanane walioteuliwa na Lipumba wataapishwa kwa kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea zuio lolote la mahakama.

Maombi ya kuzuia kuapishwa kwa wabunge wateule yaliwasilishwa Mahakama Kuu na upande unaomuunga mkono, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad.

Maombi hayo yalipingwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Gabriel Malata ambaye aliitaka Mahakama kutupilia maombi ya kuzuia wabunge hao wasiapishwe.

Uamuzi huo wa leo mchana utattolewa na Lugano Mwandambo saa nane mchana.
Wabunge waliovuliwa ubunge ni Miza Bakari Haji, Saverina Silvanus Mwijage, Salma Mohamed

Mwassa, Raisa Abdallah Musa na Riziki Shahari Mngwali, Hadija Salum Al- Qassmay, Halima Ali Mohamed na Saumu Heri Sakala wakati madiwani ni Elizabeth Alatanga Magwaja na Layla Hussein Madib.

error: Content is protected !!