Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai amtupia zigo la CUF Msajili wa Vyama
Habari za Siasa

Spika Ndugai amtupia zigo la CUF Msajili wa Vyama

Kulia Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, amesema kuwa mgogoro wa Chama cha Wananchi (CUF) wa sakata la wabunge nane ni utaratibu ulianza kwa Msajili wa Vyama vya siasa nchini na siyo bungeni, anaandika Faki Sosi.

Ndugai leo amewaambia waandishi kuwa bunge haliwezi kutiwa hatiani katika sakata hilo kwani wenye dhamana ya wanachama kutka katika vyama vya siasa ni Msajili wa Vyama vya Siasa.

Ndugai ameeleza endapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haimtambui mwanachama au kiongozi wa chama husika cha siasa naye hatamtambua kiongozi huyo.

“Mwenye kumbukumbu, Katiba na Viongozi halali wa vyombo vya siasa ni Msajili wa Vyama vya Siasa sio mtu mwengine.

“Linapotokea jambo lenye mvutano kazi yangu ni kuumuliza Msajili wa Vyama vya Siasa akisema hamfahamu basi na mimi sitamfahamu,” amesema Ndugai.

Ndugai amesema kuwa amepata barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa Mwezi, mwezi Machi mwaka huu, kwamba Maalimu Seif Sharrif Hamad hayupo Ofisi ndiyo sababu ya kutojibu barua ya katibu huyo.

Hata hivyo Ndugai amesema kuwa kwa wabunge waliopewa adhabu wasijirekebisha adhabu zitaongezeka zaidi kutokana na kuchukua na tabia za wabunge hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!