Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sheikh Ponda: Tumewasikia Lissu na Magufuli, tukaamue  
Habari za SiasaTangulizi

Sheikh Ponda: Tumewasikia Lissu na Magufuli, tukaamue  

Sheikh Issa Ponda, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
Spread the love

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amesema, Watanzania wanapaswa kuamua kati ya Tundu Lissu wa Chadema na Rais John Pombe Magufuli wa CCM nani apewe fursa ya kuongoza Taifa hilo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Sheikh Ponda ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020, kwenye mkutano wa kufunga kampeni za mgombea urais kupitia Chadema wa Lissu unaofanyika Uwanja wa Tanganyika Parkers jijini Dar es Salaam.

Amesema, katika uchaguzi mkuu kuna wagombea 15 wa urais lakini ushindani mkubwa upo kati ya Rais Magufuli na Lissu ambao kila mmoja ameweza kuongea sera zake wakizungumzia matatizo ya nchi na watakavyoyatatua.

“Leo ni siku muhimu sana ya kufanya tathimini ya kampeni ili kutusaidia kufanya uamuzi kwenye sanduku la kura. Wagombea wanaoshindana katika nafasi ya Rais kwa kiasi kikubwa ni wawili, Rais John Magufuli na Tundu Lissu.”

“Kitu muhimu ni kuhakikisha tumeelewa kwa nini tumchague huyu na tusimchague huyu. Katika kipindi cha kampeni, tupime maeneo mawili, mosi walivyoainisha matatizo ya nchi yetu na yale yatakayoleta maendeleo kwa nchi yetu,” amesema

Sheikh Ponda amesema, Rais Magufuli amebainisha Tanzania hakuna matatizo na Watanzania wanaishi vizuri, hakuna aliyepora mali yake, aliyeteswa na kila kitu kipo sawa.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

“Lakini Lissu anasema, Tanzania inapita katika kipindi kigumu cha maisha na ameainisha hakuna usalama, haki na hakuna uhuru. Kwa hiyo, ninyi mnapaswa kupima nani kati ya mgombea urais wa CCM na wa Chadema nani anazungumza ukweli,” amesema Sheikh Ponda.

Amese, amani msingi wake ni haki, “mimi nivikumbushe vyombo vya ulinzi na usalama, Watanzania wanaviheshimu sana, kwa kuwa wanaviheshimu visimamie haki ili yaliyotokea mwaka 2001 nchini Tanzania yasijirudie. Tujitokeze kupiga kura na kumchagua Yule atakayetutoa hapa tulipo kwa matatizo mbalimbali tuliyo.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania na Afrika Mashariki, Askofu Emmaus Mwamakula amesema “mimi tangu nizaliwe sijawahi kuwa mwoga” na niviombe vyombo vya dola kutenda haki.

Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, John Magufuli akihutubia mkutano wa kampeni Shinyanga

Askofu Mwamakula ameviomba vyombo vyo dola, kumwachia huru Mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ili kuwezesha kuwapo kwa haki.

Maalim Seif amekamatwa leo Jumanne asubuhi katika kituo cha kupigia kura cha Garagara na kupelekwa kituo cha Polisi Ziwani kwa mahojiano.

Askofu Mwamakula amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama “mkuu wa majeshi  na IGP Simon Sirro na makamanda wote, mkawe upande wa wananchi, msihusike na mtu yoyote alikataliwa kwa kura.

“Ninyi kazi yenu ni kuwalinda Watanzania kama wanayo haki kwa sababu ndiyo mnaowatumikia na msidhubutu kupokea amri halamu inayoweza kupoka haki za wananchi,” amesema Askofu Mwamakula

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!