Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Tuwasindikize mawakala vituoni 
Habari za Siasa

Chadema: Tuwasindikize mawakala vituoni 

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania,  kimewaomba wanachama wake kuwasindikiza mawakala wa chama hicho katika vituo vya kupigia kura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais nchini Tanzania utafanyika kesho Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Wito huo umetolewa leo Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakati akizungumza katika ufungaji kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa chama hicho, Tundu Lissu katika Uwanja wa Tanganyika Packres jijini Dar es Salaam.

“Mimi nina uzoefu wa ninyi wananchi wa Dar es Salaam, mnakawaida ya kuchelewa kupiga kura, tume imetangaza kufungua vituo saa 1:00 asubuhi, tafadhali fika saa 12:00 asubuhi kamili ,sababu wakala wetu wanawapangia njama za kutowaingiza. Akifika saa 12 asubuhi asiwe peke yake asindikizwe na wananchi kuhakikisha anaingia ndani,” amesema Mnyika.

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

Mnyika amewaomba wafuasi wa chama hicho kubaki katika vituo vya kupigia kura kusubiri matokeo yake.

“Imetolewa kauli na IGP Simon Sirro jana na leo akiwasisitiza kwamba tukipiga kura twende nyumbani, kauli iliyotolewa na mgombea wa CCM, nasema wazi na Polisi wasikie tukipiga kura hakuna kurudi nyumbani tushuhudie kazi akiendelea,” amesema Mnyika.

Mnyika amewataka wasimamizi wa uchaguzi kila mahali, watoe nakala za matokeo ngazi ya kata majimbo ili mawakala wabaki na uthibitisho wa matokeo ya uchaguzi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!