Rais John Magufuli

Rais Magufuli ateua wakili mkuu wa Serikali, Naibu wake

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa tarehe 10 Julai,2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, kabla ya uteuzi huo, Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dk. Julius Clement Mashamba.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dk. Boniface Luhende kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Luhende alikuwa Mhadhiri katika Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Malata ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Msigwa amesema,uteuzi huo wa viongozi hao unaanza leo tarehe 10 Julai, 2020.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Gabriel Pascal Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma ... (endelea). Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa tarehe 10 Julai,2020 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, kabla ya uteuzi huo, Malata alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dk. Julius Clement Mashamba. Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dk. Boniface Luhende kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Luhende alikuwa Mhadhiri katika Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!