Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto

Polisi Dodoma wawashikilia ‘machangudoa’ 22

Spread the love

WANAWAKE takribani 22 pamoja na wanaume watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya ngono. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 9 Oktoba 2018 jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Uhindini ambapo wanawake hao walikuwa wanauza miili yao wakati wanaume wawili walikuwa wateja wa baadhi ya wanawake hao.

Kamanda Muroto ameeleza kuwa, Jeshi la Polisi pia limekamata wamiliki wa baadhi ya baa zinazohifadhi ‘machangudoa’ hao.

“Tumekamata changudoa au dada poa hawa wanafanya umalaya, vile vile tumekamata baa zinazohifadhi watu hao maeneo ya Uhindini , tumekamata wamiliki wa baa na wanaume wawili. Wanaokimbilia akina dada,” amesema Kamanda Muroto.

WANAWAKE takribani 22 pamoja na wanaume watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya ngono. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Akizungumza na wanahabari leo tarehe 9 Oktoba 2018 jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Uhindini ambapo wanawake hao walikuwa wanauza miili yao wakati wanaume wawili walikuwa wateja wa baadhi ya wanawake hao. Kamanda Muroto ameeleza kuwa, Jeshi la Polisi pia limekamata wamiliki wa baadhi ya baa zinazohifadhi 'machangudoa' hao. “Tumekamata changudoa au dada poa hawa wanafanya umalaya, vile vile tumekamata baa zinazohifadhi watu…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!