Maulid Mtulia

Mbunge Mtulia chali Kinondoni, Tarimba apeta

Spread the love

MAULID Mtulia, Mbunge anayemaliza muda wake jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, ameshindwa kutetea nafasi yake katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mtulia ameangushwa na Abbas Tarimba katika kura hizo za maoni zilizofanyika leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 katika Ukumbi wa King Solomon.

Wagombea walikuwa 79 ambapo Tarimba amepata kura 171, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Iddi Azzan kura 77 na Mtulia kura 11 kati ya kura zote 404 zilizopigwa na wajumbe wote.

Wagombea wengine wamekukuta wakipata sifuri, kura moja, tatu au nne.
Matokeo hayo yametangazwa na Frank Kamugisha, msimamizi wa uchaguzi na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.

        Soma zaidi:

Katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015, Mtulia alishinda akiwa Chama Cha Wananchi (CUF) lakini tarehe 2 Desemba 2017 alitangaza kujizulu nafasi hiyo na kuhamia CCM kuunga juhudi zinazofanywa na Serikali chini ya Rais John Magufuli.

Uchaguzi uliporudiwa, CCM ilimpitisha tena Mtulia kuwania nafasi hiyohiyo na kuibuka mshindi tena akimshinda Salum Mwalimu wa Chadema.

MAULID Mtulia, Mbunge anayemaliza muda wake jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, ameshindwa kutetea nafasi yake katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea) Mtulia ameangushwa na Abbas Tarimba katika kura hizo za maoni zilizofanyika leo Jumatatu tarehe 20 Julai 2020 katika Ukumbi wa King Solomon. Wagombea walikuwa 79 ambapo Tarimba amepata kura 171, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Iddi Azzan kura 77 na Mtulia kura 11 kati ya kura zote 404 zilizopigwa na wajumbe wote. Wagombea wengine wamekukuta wakipata sifuri, kura moja, tatu au nne. Matokeo hayo yametangazwa…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

One comment

  1. Kumbe wasaliti hata CCM hawatakiwi!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!