Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Naibu Spika Tulia apeta Mbeya, Dk. Kimei chali Vunjo
Habari za Siasa

Naibu Spika Tulia apeta Mbeya, Dk. Kimei chali Vunjo

Dk. Tulia Ackson
Spread the love

NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson ameongoza katika kura za maoni Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM kwa kura 843 kati ya kura zote 885 sawana asilimia 95. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea)

Mshindi wa pili ni Mahenge Mabula aliyepata kura 16 na mshindi wa tatu akiwa ni Charles Mwakipesile aliyepata kura 11.

Iwapo, Dk. Tulia akipitishwa na chama hicho kugombea, ataumana na wagombea wa vyama vingine akiwemo Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wa Chadema.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei ameangukia pua Jimbo la Vunjo kwa kupata kura 178 akishika nafasi ya pili na aliyeongoza ni Enock Koola aliyepata kura 187 kati ya 567 zilizopigwa na wajumbe.

Charles Kimei

Nafasi ya tatu imeshikwa na Chrispine Meela aliyepata kura 47, wagombea katika kinyang’anyiro hicho walikuwa 35.

Jimbo la Ismani Mkoa wa Iringa, Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 453 kati ya 487.

William Lukuvi (wa kwanza kulia)

Wagombea walikuwa tisa ambapo aliyemfuatia amepata kura 16.

Naye mbunge anayemaliza muda wake wa Mufundi Mjini, Cosato Chumi ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 135 akifiatiwa na Bazir Tweve kura 122. 

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!