Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kupiga kura Ikungi, Magufuli Dodoma
Habari za Siasa

Lissu kupiga kura Ikungi, Magufuli Dodoma

Dk. John Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM akipiga kura Chamwino, jijini Dodoma
Spread the love

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli akiambatana na Mke wake, Mama Janeth Magufuli wamepiga kura katika Kituo cha Chamwino jijini Dodoma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wakati Dk. Magufuli akipiga kura Chamwino, mpinzani wake wa karibu ambaye ni Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu akitarajia kupiga kura Kituo cha Tewa A, Ikungi mkoani Singida.

Dk. Magufuli na Mama Magufuli wamepiga kura saa 4 asubuhi leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kituoni hapo, ambapo baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dk. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Aidha, Dk. Magufuli amewaomba Watanzania kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani.

“Wito wangu kwa Watanzania wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura kwa ajili ya maamuzi ambayo kila mmoja atakuwa nayo kwenye moyo wake, naendelea nisisitize amani tuendelee kuitunza kama Taifa sababu kuna maisha baada ya uchaguzi,” amesema Dk. Magufuli.

Kuhusu zoezi hilo, Dk. Magufuli amesema maandalizi yake mazuri hususan katika kituo ambacho yeye amepiga kura.

“Niwapongeze Watanzania wote kwa kuiona hii siku ya leo ambayo ni muhimu kukuza demokrasia katika Taifa letu. Napenda niwapongeze wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Chamwino ambacho nimepiga kura mimi na mke wangu, maandalizi yamekuwa mazuri nawapongeza kwa usimamizi mzuri,” amesema Dk. Magufuli.

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania (Chadema).

Mgombea wa Chama cha UPDP, Twalib Kadege amepiga kura mkoani Mbeya huku wa NCCR-Mageuzi , Yeremia Maganja akipiga kura katika Kituo cha Butakare Bunda mkoani Mara.

Akizungumza baada ya kupiga kura, Maganja amesema, mchakato huo kwa ngazi ya kitaifa linaendelea vizuri, isipokuwa kwa ngazi za chini kuna dosari kidogo na kutoa wito kwa wasimamizi wa uchaguzi kuendesha zoezi hilo kwa kufuata sheria na kanuni za uchaguzi.

“Tume imeendesha zoezi hili kwa uweledi mkubwa, kunaweza kuwa na tatizo kwa ngazi ya wakurugenzi lakini kwa ngazi ya taifa wamefanya vizuri nadhani walioko chini ya ukurugenzi wa hamashauri watafanya vyema, watafuata maelekezo ya tume na uchaguzi utawenda salama na watakayeshinda watamtangaza,” amesema Maganja.

Hashim Rungwe, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chaumma akipiga kura Kinondoni, jijini Dar es Salaam

Naye Kadege amesema zoezi hilo linaendelea vizuri isipokuwa mwitikio w awnanachi umekuwa mdogo.

“Katika vituo vya kupiga kura ujio wa watu haukuwa mzuri labda wana wasiwasi na vurugu lakini hakuna vurugu hali ni shwari, lakini Watanzania wanasubiri muda wa mwisho,  mwisho wa siku wanaleta malalamiko sikupiga kura,” amesema Kadege.

Kadege amewashauri wananchi kuwahi mapema kupiga kura ili kukwepa usumbufu.

Halima Mdee, Mgombea ubunge Kawe kwa tiketi ya Chadema akikwaruzana na msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo

Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo, Bernard Membe, anatarajia kupiga kura Kituo cha Londo mkoani Lindi, wakati wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe, akitarajia kupiga kura Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku wa ADC, Queen uthbert Sendiga atapiga kura katika Kituo cha Biafra-Kinondoni jijini humo.

Mgombea wa Demokrasia Makini, Cecilia Augustine Mwanga anatarajia kupiga kura katika Kituocha Kibonde Maji-Mbagala, Dar es Salaam. Mgombea wa DP, Philipo Fumbo atapiga kura Mwakizega Uvinza mkoani Kigoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!