Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Madai kura feki, Polisi wamkamata Mdee na kumwachia
Habari za Siasa

Madai kura feki, Polisi wamkamata Mdee na kumwachia

Halima Mdee, aliyekuwa ubunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni asubuhi ya leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 walimkata Mgombea Ubunge wa Kawe, Halima Mdee wa Chadema kufuatia sintofahamu iliyojitokeza katika zeozi la upigaji kura jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa zinaeleza, Mdee alikamatwa katika Kituo cha Kawe kufuatia sintofahamu hiyo kutokea baada ya mgombea huyo kudai kuona masanduku ya kura yakiwa na kura zilizopigwa kinyume na utaratibu.

Akizungumzia sakata hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Edward Bukombe amesema, mgombea huyo alihojiwa baada ya kukamatwa kisha akaachiwa huru.

Kuhusu madai ya Mdee ya sanduku kukutwa na kura za kughushi, Kamanda Bukombe amesema hawajapokea taarifa hizo.

“Mdee yuko huru, kulikuwa na tafrani ikapelekea ahojiwe lakini baadae aliachiwa huru. Chanzo ilikuwa kutoelewana,” amesema

“Kwenye uchaguzi ni kawaida  kuona mtu mabishano,  kulitokea mabishano, ilikuwa ni kituo cha Kawe, bado taarifa za kuwa masanduku yalikuwa na kura bado hatujapokea,” amesema Kamanda Bukombe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

Regina Mkonde: CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!