BAADA ya kusota mahabusu ya Magereza kwa miaka mitatu, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitiyla na wenzake, hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru leo tarehe 11 Januari, 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Shose Sinara, Mkuu wa Idara ya Uwekezaji wa Benki ya Stanbic na Sioi Solomon, Mwanasheria wa Stanbic Tanzania.
Leo Mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally watuhumia hao aliwachiwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo kama alivyopewa mamlaka na kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Wakili wa Selikali, Hashim Ngole aliieleza mahakama hiyo kuwa DDP ameamua kutoendelea na shtaka hilo.
Hakimu Ally aliamua kuwaacha huru watuhumiwa hao.
Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo kwa kosa la kuhujumu uchumi wakidaiwa kughushi nyaraka na kufanikisha uhalifu huo kati Agosti 2012 na Machi 2013 jijini Dar es Salaam.
Kosa la pili, linadaiwa kufanywa na Sinare, tarehe 2 Agosti mwaka 2012 kwa kughushi hati ya mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni katika Benki ya Stanbic ya Tanzania na Benki ya Standard ya Uingereza akiiombea fedha Serikali ya Tanzania.
Sinare anatuhumiwa kwa kosa la tatu alilotenda tarehe 13 Agosti 2012, la kupeleka hati ya kughushi kwenye Wizara ya Fedha iliyoonesha kuwa Serikali ya Tanzania itapewa mkopo wa Dola za Marekani 550 milioni kutoka Benki ya Stanbic ya Tanzania na Standard ya Uingereza.
Washitakiwa hao pia wote wanakabiliwa na kosa la kutengeneza mkataba bandia tarehe 5 Novemba, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya Benki ya Stanbic kupitia Kampuni ya Enterprise Growth Market Advisor (EGM).
Shitaka lingine linalowakabili watuhumiwa wote ni utakatishaji fedha wanalodaiwa kulitenda kati ya mwezi Machi 2013 na Septemba 2015.
Washitaki2a hao baada ya kuachiwa huru na mahakama, Polisi wamewakama tena.
Leave a comment