Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwanasiasa mkongwe awapa somo watumishi vijana
Habari za Siasa

Mwanasiasa mkongwe awapa somo watumishi vijana

Alhaji Sheikh Mohamed Mackbel
Spread the love

WATUMISHI wa serikali na taasisi mbalimbali nchini ambao bado ni vijana wametakiwa kufanya kazi zao kwa uhaminifu na uzalendo kwa faida ya jamii na taifa kwa ujumla. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa na mzee maarufu na mkongwe katika siasa Jijini Dodoma, Alhaji Sheikh Mohamed Mackbel alipokuwa juu ya mwenendo wa vijana watumishi wa serikali na sekta mbalimbali hapa nchini.

Mkongwe huyo ambaye amekuwa mtumshi kwa kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali na katika chama cha Mapinduzi kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya tano, Mackbel alisema kuwa ili kuwa na taifa imara ni
lazima liwe na vijana watendakazi wazalendo.

Alisema kuwa ni jambo la aibu na machukizo mbele za Mungu kwa mtumishi yoyote wa serikali, wa dini, pamoja na taasisi mbalimbali kufanya kazi kwa maslahi yake binafsi badala ya kutanguliza uzalendo kwa nia ya kujenga uchumi kwa faida ya maslahi mapana ya watanzania na faifa kwa ujumla wake.

Katika hatua nyingine mzee Mackbel alisema kuwa anayo fursa njema ya kuzungumza na vijana kwa njia yoyote kwa lengo la kuwataka kufanya kazi kwa maslahi mapana kwa taifa badala ya kufanya kazi kwa tamaa ya kujinufaisha wenyewe na kutaka utajiri wa haraka tofauti na kipato chake.

“Mimi nimebahatika kufanya kazi ndani ya serikali na ndani ya chama tawala tangu utawala wa serikali ya awamu ya kwanza hadi sasa kwenye utawala wa serikali ya awamu ya tano, na viongozi wote hao nimeweza kufanya nao kazi vizuri hadi sasa naendelea kufanya kazi ya siasa vizuri na serikali iliyopo madarakani.

“Msingi mkubwa ambao tuliuweka ni kuwa na nidhamu ya kazi pamoja na kuhakikisha tunakuwa wazalendo kwa kutanguliza maslahi mapana kwa faifa na jamii kwa ujumla badala ya kukimbizana kwa lengo la kutafuta masilahi binafsi.

“Wapo vijana ambao wakipata nafasi wanakuwa na jeuri na wanashindwa kuwahudumia wananchi kwa wakati na badala yake wamekuwa wakitafuta ndia ya kujipatia kipato kikubwa kwa njia ya mkato na matokeo yake wanajiingiza katika ufisadi,” alisema Alhaji Mackbeli.

Akizungumzia kuhusu viongozi wa serikali kwa maana ya marais kuanzia awamu ya kwanza hadi hivi sasa,alisema kuwa kila kiongozi amefanya vizuri kutokana na kipindi alichokiongoza na kwa maana hiyo hakuna kiongozi bora kuliko mwingine.

Akizungumzia Baba wa Taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere alisema kuwa yeye alifaya kazi kubwa ya kutafuta uhuru na kuifanya nchi kuwa utulivu jamboa ambali alisema kuwa ni jambo la muhiu hivyo ni makosa kudhani kuwa kiongozi huyo hakufanya jambo lolote.

Akizungumzia masuala ya Imani alisema kuwa viongozi wa kiimani pia wanatakiwa kutambua kuwa mchango wao ni mkubwa katika jamii na pale wanapokuwa madarakani wanatakiwa kuhakikisha wanauwaunganisha wahumini wao.

Mzee Mackbel alisema kuwa licha ya kuwa amezitumikia serikali zote akiwa mtumishi wa kiserikali na katika siasa lakini pia ameweza kupata tuzo mbalimbali za utumishi katika kupitia taasisi ya Dini ya Kiisamu kutokana na kufanya kazi kwa nia njema ya kumtumika Mungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!