Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hisia za Polepole, Zitto kwa Sumaye
Habari za Siasa

Hisia za Polepole, Zitto kwa Sumaye

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo pamoja na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamezungumzia hatua ya Frederick Sumaye, kuondoa Chadema. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Zitto amesema chama chake kimehuzunishwa na uamuzi wa Sumaye kupumzika siasa, kwa kuwa alikuwa tunu katika siasa za upinzani.

“Sisi kama chama tumehuzunishwa na uamuzi wa Mzee Sumaye kupumzika Siasa. Ilikuwa ni tunu katika upinzani kuwa na Waziri Mkuu Mstaafu katika ngazi zake za Uongozi.

“Bila shaka tutachota maarifa na uzoefu wake kama mwenyewe alivyoruhusu. Chama chetu kinaheshimu na kuthamini Wastaafu,” ameandika Zitto.

Aidha, Zitto amekitakia kheri chama cha Chadema katika uchaguzi wao wa viongozi unaotarajia kufanyika tarehe 18 Desemba 2019.

“Kwa upande wangu nawatakia kila la kheri wenzetu wa Chadema katika uchaguzi wao unaoendelea. Dhamira yetu ya kuunganisha nguvu ya Vyama vya upinzani ili kukabiliana na CCM haina mashaka. Mara baada ya Uchaguzi wa wenzetu tutaendelea na mazungumzo ya ushirikiano na Uongozi mpya,” ameandika Zitto.

Kwa upande wake Polepole kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema walimshauri Sumaye asihamie Chadema kwa madai kwamba ni mali ya mtu mmoja, lakini hakusikia.

“Mzee nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM wenzako wanaotushauri na tunazingatia ushauri wao kwasababu tunawaheshimu, ni wana CCM na kiitikadi tuko pamoja. Sasa umebaki bila Itikadi.

“Ile ni mali ya mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa unahama mara ya pili,” ameandika Polepole katika ukurasa wake wa Twitter.

Leo tarehe 4 Desemba 2019 ametangaza kuondoka Chadema kwa maelezo ya kutoridhishwa na siasa za chama hicho, hasa ukosefu wa demokrasia, kufuatia kufanyiwa figisu katika uchaguzi wa Kanda ya Pwani.

Sumaye amesema hana mpango wa kujiunga na chama chochote, na kuwa, anapumzika siasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!