Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sumaye: Wangesema ‘usiguse hapa’
Habari za Siasa

Sumaye: Wangesema ‘usiguse hapa’

Spread the love

FREDERICK Sumaye, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, amelalamika kutoelezwa ‘ukweli,’ kwamba uchaguzi wa ngazi ya uenyekiti kwenye chama hicho, haufuati Katiba ya chama. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akitangaza kujiondoa kwenye chama hicho leo tarehe 4 Desemba 2019, Sumaye amesema hakujua kuwa nafasi ya uenyekiti ndani ya chama hicho ‘ina mwenyewe.’

“Basi wangenitahadharisha katika chama chetu, utaratibu wa uenyekiti uko nje ya Katiba, ningeelewa,” amesema Sumaye.

Amesema, kilichomuondoa Chadema ni ukosefu wa demokrasia “ni pamoja na kufanyiwa figisu kufuatia hatua yangu ya kutangaza kugombea uenyekiti wa chama hiki.”

Amesema, kujitosa kwake kugombea uenyekiti, kulizua nongwa n ahata kufedheheshwa kwenye uchaguzi wa Kanda ya Pwani, kutokana na mkakati uliopangwa.

“Kwa kitendo hiki kilichotengenezwa na wenzangu wa Chadema, nimefedheheka sana, hasa kwa kuonekana  nimekosa adabu kwa kutaka kugombea uenyekiti wa Chadema,” ameeleza Sumaye.

Ameeleza kuwa, aliamua kugombea uenyekiti ili kuondoa dhana ya kwamba ndani ya Chadema hakuna demokrasia, na pia nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ni ya Mbowe, ambayo haitakiwi kuguswa na mtu yeyote.

“Nongwa ilikuja baada ya mimi kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chetu. Lengo nilitaka kuondoa hisia iliyojengeka kwenye jamii kwamba ndani ya Chadema hakuna demokrasia ya kweli. Nafasi ya uenyekiti wa Chadema ni ya Mbowe haiguswi na mtu yeyote,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!