Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM

CCM yaiga staili ya upinzani

Spread the love

KAULI zilizokuwa zikitolewa na vyama vya upinzani nchini Tanzania kwamba ‘tutalinda kura zetu,’ sasa zinatolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, CCM italinda kura zake. Jukumu la ulinzi wa kura hizo limeelekezwa kwa taasisi yake ya vijana – Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tarehe 3 Agosti 2020 aliwaeleza wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho kwamba, watalinda kura zao.

Pia, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo akihutubia Kikao cha Halmashuri Kuu ya chama hicho kilichoketi tarehe 3 Agosti 2020, katika Ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam alisema, chama hicho kitalinda ushindi wake na hakitakuwa tayari kuporwa.

Kauli ya Dk. Bashiru aliyoitoa leo Alhamisi tarehe 6 Agosti makao makuu ya CCM kwamba, chama hicho kitalinda kura zake inafanana na zile zilizotolewa na Chadema pia ACT-Wazalendo.

Maalim Seif, M/kiti ACT-Wazalendo Taifa

“Tuache maneno yao ya mdhaha, sisi ni watu wa kazi ya maendeleo kwa Taifa letu. Natamka, mitambo ya ushindi imewashwa rasmi leo, ule wa kutesti mitambo umeisha, na mitambi hiyo tumekabidhi CCM.”

“Kazi yakutafuta kura na kuzilinda, kuwalinda wapiga kura na kuhamasisha wapiga kura, nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda tunawakabidhi Umoja wa Vijana wa CCM,” amesema Dk. Bashiru.

Pia, amesema, pamoja na chama hicho kufungua rasmi mitambo yake, Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT), inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Gaudensia Kabaka itakuwa ndio inalainisha mitambo hiyo.

“Lakini mitambo hii ni ya kiasasa, inahitaji mafuta, ukarabati, maji ya kupoza poza kama ikipata joto, kazi hiyo ni ya kina mama wa CCM,” amesema.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Dk. Bashiru amesema, “lazima mitambo iwe na kiongozi, dereva wa kushika breki kwenye mteremko, kutokutoa rushwa kwa trafiki barabarani, siku 60 za kampeni, tunawakabidhi Umoja wa Wazazi Tanzania. Ushindi wa mwaka huu ni wa kishindo kikubwa.”

Katibu Mkuu huyo amesema, Dk. Magufuli amepitishwa kuwa mgombea urais wa chama hicho kutokana na utii wake, unyenyekevu wake, msimamo wake kuhusu maslahi ya nchi

“Mkutano Mkuu wa CCM umezingatia rekodi yako ya utumishi wa serikali kwa zaidi ya miaka 20, tangu ubunge, waziri wa wizara mbalimbali hasa Wizara ya Ujenzi.

“Wewe ni mtu wa watu, mnyenyekevu, kimbilio la wanyonge, kiboko cha mafisadi na wala rushwa. Ni mkali kwa maovu, ni tishio kwa mabeberu. Kutokana na msimamo wako, Tanzania sasa si shamba la bibi tena,” amesema.

KAULI zilizokuwa zikitolewa na vyama vya upinzani nchini Tanzania kwamba ‘tutalinda kura zetu,’ sasa zinatolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, CCM italinda kura zake. Jukumu la ulinzi wa kura hizo limeelekezwa kwa taasisi yake ya vijana - Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM). Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tarehe 3 Agosti 2020 aliwaeleza wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho kwamba, watalinda kura zao. Pia, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo akihutubia Kikao…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!