Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo, Yassin  Mohammed

ACT-Wazalendo yawatumia salamu watakaoiba kura

Spread the love

MWENYEKITI wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo, Yassin  Mohammed amesema, mwenyezi Mungu atawaadhibu watakaoshiriki wizi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Yassin ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020, kwenye uzinduzi wa kampeni za Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Saed Kubenea katika Viwanja vya Buibui Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mzee Yassin amesema, maombi yanayofanya na mtu aliyedhulumiwa hukubaliwa na mwenyezi Mungu haraka.

“Mtu yoyoye atakayedhulumu haki yetu awe ndani ya chama chetu au chama kingine au msimamizi wa uchaguzi mwenyezi Mungu atamuadhibu,” amesema Yassin.

Wakati huo huo, Yassin amewataka wananchi wa Kinondoni kutochagua viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwa hawaweki maslahi ya wananchi mbele badala yake wanailinda Serikali .

MWENYEKITI wa Ngome ya Wazee ya ACT-Wazalendo, Yassin  Mohammed amesema, mwenyezi Mungu atawaadhibu watakaoshiriki wizi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Faki Sosi ...(endelea). Yassin ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020, kwenye uzinduzi wa kampeni za Mgombea Ubunge wa Kinondoni, Saed Kubenea katika Viwanja vya Buibui Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mzee Yassin amesema, maombi yanayofanya na mtu aliyedhulumiwa hukubaliwa na mwenyezi Mungu haraka. https://youtu.be/YHmWaSZmvI8 "Mtu yoyoye atakayedhulumu haki yetu awe ndani ya chama chetu au chama kingine au msimamizi wa uchaguzi mwenyezi Mungu atamuadhibu," amesema Yassin. Wakati huo huo, Yassin amewataka…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!