Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sheikh Katimba: 28 Oktoba fursa wapinzani kupumua
Habari za Siasa

Sheikh Katimba: 28 Oktoba fursa wapinzani kupumua

Sheikh Rajab Katimba kutoka Taasisi ya na Jumuiya za Kiislamu Tanzania
Spread the love

SHEIKH Rajab Katimba kutoka Taasisi ya na Jumuiya za Kiislamu Tanzania amesema, Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 utumike kama fursa ya upinzani nchini humo kupumua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Sheikh Katimba amesema hayo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 katika uzinduzi wa kampeni za Mgombea Ubunge wa  Kinondoni kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Saed Kubenea uliofanyika Viwanja vya Buibui jijini Dar es Salaam.

Amesema, vitendo vya vyama vya upinzani kuhujumiwa katika michakato ya uchaguzi vinapaswa kukomeshwa kwa kuiondoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani kupitia uchaguzi huo.

https://youtu.be/YHmWaSZmvI8

“Wapinzani ndio wenye kushughulikiwa,  kuenguliwa wao. Tumeshuhudia mwaka jana wapinzani wamebanwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hii sio fursa ya kuichezea, inatakiwa kila mtu kuitumia kura yake kuhakikisha ufisadi tunauondoa sababu Mungu hapendi ufisadi,” amesema  Sheikh Katimba.

Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2019, CCM ilishinda uchaguzi huo kwa zaidi ya asilimia 95 baada ya baadhi ya vyama vya upinzani kususia uchaguzi huo kutokana na wagombea wake wengi kuenguliwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokidhi masharti ya ujazaji fomu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!