April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zitto awapa tano Tundu Lissu, Mbowe

Spread the love

ZITTO Kabwe Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amempongeza Freeman Mbowe, kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti  wa Chadema na Tundu Lissu kuwa Makamo Mwenyekiti wa Chama hicho. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Salamu hizo zilizotolewa na Ado Shaibu Katibu wa Itikadi Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo, zimeleza kuwa Zitto na chama chake kinakipongeza Chadema kwa kufanikiwa kufanya mkutano mkuu, sambamba na kuchagua viongozi wao. 

Zitto amewahakikishia viongozi hao kuwa chama chake kitashikirikiana na Chadema na vyama vingine vyenye dhamira ya kuitetea na kupigania demokrasia.

Chadema kinataraji kuhitimisha kikao chake leo kwa kuteua nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho sambamba na manaibu makatibu wakuu Bara na Zanzibar.

error: Content is protected !!