November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto atoka hospitalini ‘narudi kwenye kampeni’

Spread the love

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Aga Khani jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Zitto na watu wengine wanne walipata ajali ya gari akitoka Kata ya Kalya kwenda Lukoma kwenye mkutano wa kampeni Jimbo la Kigoma Kusini 6 Oktoba 2020.

Baada ya kutokea kwa ajali hiyo, majeruhi wote walipatiwa huduma ya kwanza Kituo cha Afya cha Kalya kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma na baadaye Hospitali ya Aga Khan.

Leo Jumamosi tarehe 10 Oktoba 2020, Zitto ameandika katika ukura wake wa Twitter ameandika “nimeruhusiwa kutoka hospitali. Nawashukuru madaktari na wauguzi Kituo cha Afya Kalya – Uvinza, Hospitali ya Maweni Kigoma na Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam.”

Zitto ambaye ni mgombea ubunge wa Kigoma Mjini amesema “asanteni sana wote kwa Dua, Sala na maombi yenu. Nataraji kurudi kwenye kampeni siku chache zijazo In Sha Allah.”

error: Content is protected !!