May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NEC yaweka masharti matumizi ya simu vituoni Oktoba 28

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imeweka masharti ya matumizi ya simu katika vituo vya kuhesabu, kupigia na kujumulishia kura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Masharti hayo ni miongoni mwa Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 yaliyotolewa na NEC ikielezea mambo sita yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa wakati wa upigaji kura mpaka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Mambo hayo yasiyotakiwa ni;

Mosi; mtu yeyote kutumia simu ya kiganjani ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura isipokuwa msimamizi wa kituo, wasaidizi wake na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao watatumia simu zao pale itakapobidi kwa shughuli za uchaguzi tu na simu hizo wakati wote ziwe zimeondolewa mlio na ziwe kwenye mtetemo.

          Soma zaidi:-

Pili; viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha fujo, vurugu katika vituo vya kupigia, kuhesabu na kujumlishia kura.

Tatu; vyama vya siasa, wagombea na wafuasi wao katika siku ya kupiga kura kufanya  kampeni ya aina yoyote ikiwa ni pamoja na kuvaa vazi lolote au kuwa na kitu chochote kinachoashiria kushawishi watu kumpigia kura mgombea Fulani.

Hii ni pamoja na matumizi ya vyombo vya usafiri vilivyokuwa vinatumika wakati wa kampeni vinavyoashiria utambuzi wa chama Fulani.

Nne, kiongozi, mgombea au mtendaji yeyote wa chama cha siasa kutoa lugha ya matusi kwa mtendaji wa uchaguzi.

Endapo kuna changamoto au lalamiko lolote kuhusiana na mchakato au taratibu za uchaguzi katika kituo cha kupigia kura, changamoto hizo zitawasilishwa kwa maandishi kwa msimamizi wa kituo kupitia kwa wakala.

Tano; kiongozi au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kuvamia au kukaa kwa nguvu ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia au kujumlishia kura.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

Sita; kiongozi, mgombea au mtendaji wa chama cha siasa, mwanachama au mfuasi kujihusisha na vitendo vifuatuvyo;
I; kuwahamasisha wanachama au wafuasi kupiga kura zaidi ya mara moja katika uchaguzi mmoja
II; kununua kadi ya mpiga kura, kununua kura au kutoa hongo, zawadi, shukrani au aina yoyote ya malipo ya fedha au vifaa kwa mpiga kura au mtendaji wa uchaguzi.

error: Content is protected !!