Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aichongea CCM kwa wananchi
Habari za Siasa

Zitto aichongea CCM kwa wananchi

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo amewataka Watanzania wasikipigie kura Chama Chama Mapinduzi  (CCM) kwani kimeshindwa kutekeza ahadi walizoahidi kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. Anaaripoti Faki Sosi, Lindi … (endelea)

Zitto amesema, CCM imekuwa akiahidi lakini haitekelezi na uchaguzi mwingine unapofika inaahidi tena jambo ambalo amewaomba Watanzania siku ya uchaguzi mkuu tarehe 28 Oktoba 2020 kuiweka kando.

Kiongozi huyo wa chama, amesema hayo katika uzinduzi wa kampeni za urais wa chama hicho leo Jumanne tarehe 1 Septemba 2020 katika Viwanja vya Mpilipili  Mjini Lindi.

ACT-Wazalendo, imemsimamisha Bernard Membe kuwania urais na Profesa Omar Fakih Hamad, mgombea mwenza.

“CCM iliahidi mikoa ya kusini itakuwa na uchumi wa gesi lakini mpaka sasa haijulikani hili limeishia wapi, Je, watu wa Lindi  mmeuona uchumi wa gesi, watu ambao hawakutekeleza ahadi yao mtawachagua tena,” amehoji Zitto na kujibiwa ‘hapana, haiwezekani.

Zitto amesema, CCM ilitoa ahadi ya kutoa Sh. 50 milioni kila kijiji  “lakini hakuna kijiji hata kimoja kilichopata fedha na hawa hawa CCM waliahido kutoa ajira milioni moja lakini hawakutekeleza, hivi karibuni wameahidi kutoa kajira milioni sita nazo itakuwa vile vile.”

Amesema kutokana na hilo, chama hicho kimeandaa Ilani itakayonadiwa na mgombea wake wa urais, Membe na mgombea mwenza, Profesa Hamad ambayo ni mkombozi wa wananchi wote.

Zitto ambaye ni mgombea ubunge Kigoma Mjini amesema, katika kipindi cha siku 62 za kampeni, watazunguka nchi nzima kuinadi ilani hiyo kwa Watanzania ili waweze kuwachahua na kuongoza dola.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!