October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zengwe la Meya Dar lahamia Meya Iringa

Alex Kimbe, Meya wa Manispaa ya Iringa

Spread the love

MKAKATI ulioondeshwa na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka kumng’oa Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam sasa umehamia kwa Alex Kimbe, Meya wa Manispaa ya Iringa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Sakata la kumng’oa Meya Kimbe (Chadema), limeshika kasi ambapo sasa, amepewa siku tano ya kujieleza na hatimaye kufanyika kikao ili kumng’oa madarakani.

Tayari Kimbe ameandikiwa barua ya kujieleza ndani ya siku tano ikibeba tuhuma nne ambazo ni ukosefu wa adabu, matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri na vitendo vya rushwa.

Akizungumza na wanahabari tarehe 2 Machi 2020, Meya Kimbe amesema amepokea barua iliyobeba tuhuma hizo za kupikwa kwa sababu maalum za kisiasa.

Yeye mwenewe ameeleza, kwamba leo tarehe 3 Machai 2020, atawasiliana na mkurugenzi wa halmashaui hiyo Hamid Ahmed Njovu, kumweleza namna taratibu za barua hiyo zilivyokwenda hovyo.

“Nitapeleka barua kwa mkurugenzi wa manispaa ili nimweleze na kumkumbusha vyombo vya usalama na watendaji wake taratibu na kanuni za kumtoa Meya madarakani wamezikosea,” amesema.

Meya Kimbe amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekosa fursa kwa wananchi na sasa kinatumia hila kukabili maeneo yanayoongozwa na wapinzani ikiwemo Manispaa ya Iringa.

“Nikiona mkurugenzi hanipo majibu yanayojitosheleza, nitakwedna mahakamani,” amesema Meya Kimbe na kuongeza “

Barua hiyo iliyosainiwa na Njovu, imeeleza dhamira ya kuwepo kwa kikao cha madiwani ambacho kinaweza kudhamiria kumng’oa madarakani kutokana na tuhuma hizo.

error: Content is protected !!