April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif amfuata JPM Ikulu

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ametinga Ikulu, jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Muda mfupi baada ya kukutana na Rais Magufuli leo tarehe 3 Machi 2020, Maalim Seif ameeleza kuwa wamezungumzia masuala ya nchi na namna ya kufanya amani iendelee kuwepo.

“Tumekutana na kubwa tumezungumzia mambo ya nchi yetu, vipi tutaendelea kuifanya Tanzania iwe na amani, nchi ya salama na upendo kwa Watanzania wote,” amesema Maalim Seif na kuongeza:

“Ni mtu muwazi na anapenda kukutana na watu, nafurahi sana kwa rais anakubali kukutana na raia wake…, namshukuru rais kakubali tukutane, tuzungumze mambo ya maslahi ya nchi yetu.”

Hata hivyo, Maalim Seif ameeleza kwamba, mengine aliyoongea na rais yatabai ndani na hayawezi kupelekwa kwa jamii “mengine tumezungumza humo ndani mimi na rais, huwezi kuyasema public (wazi), bila shaka kukiwa na haja ya kukutana, tutakutana tena.”

error: Content is protected !!