April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lema: Polisi wananisaka

Spread the love

GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini amedai kwamba, anatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Lema ametoa taarifa hiyo leo tarehe 2 Machi 2020, kupitia ukurasa wake wa twitter, huku akidai kwamba, amepigiwa simu ya wito wa kwenda Ofisini kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi (RCO) wa mkoa huo.

Hata hivyo, Lema amedai kuwa, kabla ya kupigiwa simu ya wito wa kwenda polisi, askari kanzu kadhaa walikwenda nyumbani kwake kumtafuta, lakini hawakumpata.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini amesema, hadi sasa hajajua sababu za wito huo, na kwamba anawasiliana na mawakili wake kwa ajili ya kwenda ofisini kwa RCO.

“Nimepata taarifa kuwa gari mbili za Polisi zikiwa na askari kanzu zime kwenda kunitafuta nyumbani kwangu bila taarifa,wamenikuta nimeondoka,hivyo nimepigiwa simu na kutakiwa ofisi ya RCO Arusha.Hawajataka kusema wana nitafutia nini?nina wasiliana na Wakili wangu kuelekea,” ameandika Lema katika ukurasa wake wa Twitter.

MwanaHALISI Online ilimtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha, kwa ajili ya ufafanuzi wa suala hilo, lakini muda wote simu yake ilijibu inatumika.

error: Content is protected !!