Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Z’bar maambukizi ya corona yapanda
AfyaHabari Mchanganyiko

Z’bar maambukizi ya corona yapanda

Hamad Rashid Mohammed, Waziri wa Afya Zanzibar.
Spread the love

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya sita wa Homa Kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa ya ongezeko hilo imetolewa leo tarehe 15 Aprili 2020, na Hamad Rashid Mohammed, Waziri wa Afya Zanzibar.

Taarifa ya Mohammed inaeleza kuwa, kufuatia ongezeko hilo, kwa sasa Zanzibar ina jumla ya wagonjwa 18 kutoka idadi ya watu 12 iliyokuwepo awali.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wagonjwa watano ni raia wa Tanzania ambao hawana historia ya kusafiri nje ya nchi siku za hivi karibuni, na mmoja ni raia wa Misri, aliyeingia nchini akitokea kwao kupitia Dubai kwa Shirika la Ndege la Fly Dubai.

Mohammed amesema wagonjwa wote wamelazwa katika vituo maalumu kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

“Serikali kupitia wizara ya afya inaendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huu zinazotolewa mara kwa mara ikiwemo unawaji mikono kwa maji yanayotiririka na sabuyni , kuepuka misongamano na kuahirisha safari za nje na ndani ya nchi zisizo za lazima,” inaeleza taarifa ya Mohammed.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!