Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Zawadi NMB MastaBata kuwakwamua wateja kiuchumi
Habari Mchanganyiko

Zawadi NMB MastaBata kuwakwamua wateja kiuchumi

Spread the love

MSIMU wa nne wa kampeni ya NMB MastaBata tayari umeanza baada ya promosheni hiyo ya kuchagiza malipo kidijitali kuzinduliwa Mbeya huku sehemu ya zawadi zenye thamani ya Sh350 milioni ikipangwa kutumika kuwawezesha wateja kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kiasi cha Sh173 milioni na pikipiki 14 zitatumika kuwakwamua kiuchumi washindi wa shindano hilo linalojulikana mara hii kama NMB MastaBata, Kote-Kote!

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi utaratibu huo utasaidia kuimarisha vipato vya wateja watakaoibuka washindi

Alisema MastaBata ya mwaka huu itaua ndege wawili kwa jiwe moja. Itahamasisha matumizi zaidi ya kadi za NMB Mastercard and Masterpass QR (lipa mkononi) na kuwapa fursa wateja kuboresha hadhi zao kiuchumi.

“Tofauti na mwaka jana, mwaka huu tumeamua kuwa na zawadi ya fedha pamoja na pikipiki sababu tunahitaji sio tu kuhamasisha matumizi ya kadi lakini pia kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi ya wateja wetu, tunaamini pikipiki hizi zinakwenda kutumika katika biashara na kuongeza kipato cha washindi wetu,” alisema Mponzi

Zawadi kubwa itakayohitimisha kampeni ya NMB MastaBata, Kote-Kote ni washindi saba kujishindia tiketi za kusafiri kwenda Dubai pamoja na wenzi wao kwa siku nne.

Pia, zitakuwepo droo za kila wiki na kila mwezi na shindano hilo litaendeshwa kwa wiki 10.

“Jumla ya shilingi milioni 350 zitatolewa kama zawadi kwa washindi 854,” alisema Mponzi na kubainisha shughuli hiyo ni miongoni mwa michakato ya kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wateja.

Kupitia zawadi hizo, NMB inataka na msimu unaokuja wa Krismasi na Mwaka Mpya kufana zaidi kwa wateja wake, na kusema kwani kila wiki wateja 75 watajishindia TZS 100,000 kila mmoja.

Jumla watanyakua Sh7.5 milioni na shindano litakapotamatika Januari 2023 zawadi hiyo itakuwa imefikia Sh 75 milioni. Kila baada ya siku 28 kwa miezi miwili mfululizo washindi 49 wataibuka na Sh1 milioni kila mtu ambazo ni sawa na Sh49 milioni kila droo na Sh 98 milioni kwa droo zote mbili.

Kila wiki kutakuwa na zawadi ya pikipiki moja na mbili kila mwezi na jumla zitakuwa pikipiki 14 kampeni itakapomalizika.

Mgeni rasmi wa uzinduzi huo likuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Rashid Chuachua, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Juma Homera.

Kiongozi huyo alisema uwekezaji ambao NMB inaufanya ni sahihi kwa ulimwengu wa sasa hivi wa kidijitali na uchumi wa dunia unaoendelea kupunguza matumizi ya fedha taslimu.

Chuachua alisema kupitia NMB, Mbeya na Tanzania yote kwa ujumla imepata mshirika wa dhati wa maendeleo aliyetayari kuchangia ustawi wa jamii.

Alisema mfano mzuri wa NMB kuwa tayari kuwajibika kwa jamii ni mabati 600 na madawati 400 iliyozichangia shule tano za Mbeya mwezi Julai mwaka huu.

Huu ni mwaka wa wanne wa mfululizo wa kampeni za NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Mastercard kuhamasisha malipo bila kutumia pesa taslimu. Mchakato huu ulianza na MastaBata mwaka 2018, kisha MastaBata Sio Kawaida na kampeni ya mwaka jana ilikuwa ni MastaBata – KivyakoVyako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!