December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wahudhuria uzinduzi makao makuu ya ACT-Wazalendo

Spread the love

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimehudhuria uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya Chama cha ACT-Wazalendo lililopewa jina la Maalim Seif Sharif Hamad lililopo Magomeni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam… (endelea).

Chadema imewakilishwa na Makamu Mwenyekiti Taifa Zanzibar,  Salum Mwalimu ambaye ameungana na viongozi wa kitaifa wa ACT-Wazalendo katika kuzindua na kakagua jengo hilo lililopo Mtaa wa Mbweni karibu na ilipo nyumba ya makumbusho ya Baba wa Taifa,  Julius Nyerere. Vyama vingine vilivyohudhuria ni pamoja na NCCR-Mageuzi na ADC.

Chadema imehudhuria uzinduzi huo licha ya kuwepo kwa mjadaala mkali na kutupiana maneno miungoni mwa viongozi wa chama kuhusu ukubwa wa ofisi hiyo ikilinganishwa na ile ya kwao iliyopo Mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mbali na vyama vya siasa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumapili tarehe 30, Oktoba,  2022, umehudhuriwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa,  Sisti Nyahoza,  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku na Mwakilishi wa Ubalozi wa Uingereza.

error: Content is protected !!