Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zao la mkonge, Majaliwa atoa maagizo
Habari za Siasa

Zao la mkonge, Majaliwa atoa maagizo

Zao la mkonge
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameziagiza Halmashauri zinazolima mkonge nchini pamoja na wakulima wakubwa wa mkonge, watenge ekari kumi kwa akili ya kuanzisha vitalu vya kuzalisha miche ya mkonge ili kupunguza tatizo la upungufu wa mbegu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea)

Pia, Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo itenge fedha katika bajeti yake kwa ajili ya kituo cha TARI Mlingano lengo ni kukiwezesha kupanua eneo la uzalishaji miche kwa kununua vitendea kazi yakiwemo matrekta.

Ametoa maagizo hayo leo Jumatano, tarehe 20 Januari 2021, baada ya kukagua kitalu cha miche ya mkonge la TARI Mlingano lililopo wilayani Muheza, Tanga na kufungua zoezi la ugawaji wa miche kwa wakulima wa zao hilo.

Amesema ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa miche ya mkonge nchini, kila halmashauri na wakulima wakubwa wanatakiwa watenge ekari 10 kwa ajili ya kuandaa vitalu vya miche ya mkonge na kugawa kwa wananchi kwenye maeneo yao.

Majaliwa amesema, kituo cha TARI Mlingano kinatakiwa kijikite katika kufanya utafiti wa mbegu bora pamoja na dawa za kudhibiti magonjwa katika zao hilo na suala la uzalishaji wa mbegu lifanywe kwa ushirikiano katika ya kituo hicho na wadau wa zao hilo.

Kadhalika, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha mpaka ifikapo mwakani kuwa na ongezeko la uzalishaji wa miche zaidi ya Milioni mbili ya sasa kwani mahitaji ni makubwa kwa sasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mlingano, Dk. Catherine Senkoro amesema, hadi kufikia Januari, 2021 jumla ya hekta 32.6 sawa na ekari 81.5 zimepandwa miche ya mkonge katika maeneo ya TARI Mlingano.

Amesema kituo chao kwa kushirikiana na Bodi ya Mkonge Tanzania, imetoa mafunzo kwa wakulima na Maafisa Ugani katika baadhi ya mikoa inayofaa kwa kilimo cha mkonge ambayo ni Tanga, Morogoro, Pwani, Kilimanjaro, Lindi, Simiyu, Shinyanga na Mara.

“Kufikia Desemba 2020, wakulima 422 na Maafisa Ugani 840 katika mikoa hiyo walipatiwa mafunzo,” alisema.

Mkurugenzi huyo amesema, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Wizara ya Kilimo kupitia kituo cha TARI Mlingano imepanga kuzalisha miche 4,000,000 katika vitalu vyake, pia itapanua maabara ya uzalishaji wa miche kwa njia ya chupa ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa miche. Utaratibu huo unakadiriwa kuchangia miche milioni 10 kwa mwaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!