May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi ajinyoga ndani mwake

Kitanzi

Spread the love

ASKARI wa Kituo cha Polisi Kibaha mkoani Pwani, Yusuph Mohamed Said (52), amekutwa amejinyonga nyumbani kwake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea). 

Taarifa ya tukio hilo, imetolewa jana Jumanne tarehe 19 Januari 2021, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, wakati anazungumza na wanahabari mkoani humo.

Akielezea tukio hilo, Kamanda Nyigesa amesema, limetokea jioni ya tarehe 18 Januari 2021.

“Askari wa cheo cha Koplo namba E6472, Yusuph Mohamed Said, ana miaka 52, alikuwa anafanya shughuli za uaskari katika Kituo cha Polisi Kibaha.”

“Tarehe 18 Januari 2021 majira ya saa 12 jioni, amekutwa katika nyumba yake inayoendelea na ujenzi, akiwa amejinyonga,” alisema Kamanda Nyigesa.

Kamanda Nyigesa alisema, uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanywa na Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa (katikati)

Alisema Jeshi la Polisi mkoani humo linafanya maandalizi ya kuusafirisha mwili wake kwenda kwao mkoani Lindi, kwa ajili ya mazishi.

“Jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi wa kifo hiki cha marehemu.  Tunafanya maandalizi ya kumsafirisha kwao mkoani Lindi kwa mazishi,” alisema Kamanda Nyigesa.

error: Content is protected !!